Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam Sayyid Dhia al-Hasan Najafi katika khutba za Sala ya Ijumaa zilizosomwa kwenye Msikiti Mkuu wa Ali mjini Lahore, Pakistan, huku akielezea juhudi za baadhi ya watu katika kutaka kumtakasa Yazid dhidi ya jinai za Karbala, alisisitiza kuwa kumlaani Yazid si kwa mtazamo wa Kishia tu, bali pia kunakubalika na kukubaliwa kwa mujibu wa maoni ya wanazuoni wengi wa Ahl al-Sunnah.
Akiwa na huzuni juu ya mwenendo usio sahihi unaooneshwa na baadhi ya watu katika historia, alisema kwamba: Kwa bahati mbaya, watu wengi huunda itikadi zao kwa misingi ya dhana na mwelekeo wa kibinafsi, kisha hujaribu kuhalalisha na kuthibitisha mitazamo hiyo kwa aya za Qur’ani na Hadithi, hili ni janga la kiakili na kidini ambalo linaendelea hadi leo.
Mwanazuoni huyu kutoka Pakistan, huku akikosoa vikali juhudi kadhaa za kutaka kumtakasa Yazid kutokana na jinai kubwa ya Karbala, alibainisha kuwa: Hivi leo, baadhi ya watu wanajitahidi kumwondolea Yazid jukumu la mauaji ya Imam Hussein (as). Wanadai kuwa mauaji hayo yalikuwa ni uamuzi binafsi wa Ibn Sa’ad na kwamba Yazid hakuwa na nafasi yoyote katika hilo, na wakati mwengine, wanakataza kumlaani Yazid na wanamuweka miongoni mwa watu watakatifu, Hali ya kuwa nyaraka za kihistoria zilizo thabiti – hasa zile zilizopokewa ndani ya Tārīkh al-Ṭabarī – kwa uwazi mkubwa zinathibitisha kinyume cha madai hayo.
Maoni yako